Benki ya Mkombozi imefungua tawi mkoa wa Kagera, Desemba 15, 2015. Tawi hilo lilizinduliliwa na Askofu wa Jimbo la Bukoba, Mhashamu Desiderius Rwomo.
 
Hii ni fursa kwa wakazi mjini Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla kufaidi huduma zinazotolewa na banki hii inayokua kwa kasi.
 
Miongoni mwa fursa hizo ni mikopo ya wajasiriamali wadogo na wakubwa, mikopo ya kampuni, mikopo ya wafanyakazi, ufunguaji wa akaunti za akiba na za muda maalumu.
 
Ni fursa pia kwa wakazi wa Kagera kuimiliki benki hii kwa kununua hisa ili kufaidi gawio la faida kulingana na biashara ya benki hii.

Benki ya Mkombozi imeanza kufungua matawi maeneo mbalimbali baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuridhika na namna inavyojiendesha na kuinua uchumi wa nchi.
 
Ni Benki iliyoanza kufanya kazi nchini Agosti 28, 2009 ikiwa na tawi moja la St. Joseph lililopo Potsa ya zamani  kitalu namba 40, mtaa wa Mansfield. Tangu kuanza kwake, Benki imekuwa ikifanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.
 
Mpaka sasa ina matawi  sita  nchini. Matawi mengine yapo Mwanza, Moshi, Msimbazi Centre  na Kariakoo.
 
Kwa kuwa ukuaji wa Benki kwa sasa ni mzuri ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Kagera, kushiriki katika kufurahia matunda ya benki hii kwa kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kutumia huduma za kibenki kwa faida yao na uchumi wa Taifa kwa jumla.
 
Benki ya Mkombozi ilianzishwa na Kanisa Katoliki na sasa inamilikiwa na wananchi, kwa mtindo wa kununua hisa, bila kujali imani za dini wala kabila.