TAARIFA KWA WANAHISA WA BENKI YA BIASHARA MKOMBOZI
TAARIFA KWA WANAHISA WA BENKI YA BIASHARA MKOMBOZI
Taarifa inatolewa kwamba; Mkutano Mkuu wa Kumi na Mbili wa Wanahisa wa Benki ya Biashara Mkombozi utafanyika tarehe 31 Julai, 2021, kwenye Kituo cha Msimbazi, Ukumbi wa Kardinali Adam, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi.
Ajenda
12.1 Kufungua mkutano;
12.2 Kuridhia ajenda za mkutano;
12.3 Kuthibitisha kumbukumbu za Mkutano Mkuu wa kumi na moja wa mwaka uliofanyika tarehe 12 Septemba, 2020;
12.4 Kupokea na kujadili yatokanayo na taarifa ya Mkutano Mkuu wa kumi na moja wa mwaka wa wanahisa uliofanyika tarehe 12 Septemba, 2020;
12.5 Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya Bodi ya Wakurugenzi kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba, 2020;
12.6 Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya fedha ya benki kwa mwaka ulioishia tarehe 31 Disemba, 2020; na kupokea ripoti ya mkaguzi wa nje wa hesabu, juu ya taarifa hiyo ya fedha.;
12.7 Kuteua mkaguzi wa nje wa hesabu za benki;
12.8 Kupokea tarifa ya maendeleo ya kuongeza mtaji wa benki
12.9 Uchaguzi wa Wakurugenzi
12.10 Kupanga tarehe ya mkutano mkuu wa mwaka ujao;
12.11 Mengineyo; na
12.12 Kufunga mkutano
Angalizo:
- Mwanahisa anayetaka kushiriki katika mkutano huu ni lazima aje na nakala ya risiti yake ya ununuzi wa hisa au cheti cha hisa cha kumtambulisha kuwa ni mwanahisa.
- Mwanahisa mwenye stahili ya kuhudhuria mkutano huu ana haki ya kumteua mwakilishi wake wa kupiga kura kwa niaba yake kwa mujibu wa taratibu za kampuni. Fomu husika inayopaswa kujazwa na Mwanahisa kwa ajili ya uteuzi huo inatakiwa kufikishwa kwa katibu wa benki siku tatu kabla ya mkutano. Fomu hiyo iandikwe kama ifuatavyo: -
“Benki ya Biashara Mkombozi”
Mimi/Sisi.......................……………...................., wa ......................................................,nikiwa/tukiwa Mwanahisa/Mjumbe wa Kampuni iliyotajwa hapo juu, namteua/tunamteua ................................................................................ wa ......................................................... kama mwakilishi wangu/wetu kupiga kura kwa niaba yangu/yetu katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wanahisa wa Benki utakaofanyika tarehe 31 Julai, 2021
Saini .........................................
Imetolewa leo tarehe .............. Mwezi ………….. 20…...
- Wanahisa wote au wawakilishi wao wanahitajika kujisajili kwanza kabla ya kuingia kwenye ukumbi siku ya mkutano.
- Vitabu vya taarifa ya hesabu za benki vitakuwepo katika matawi ya benki wiki moja kabla ya mkutano.
Kwa taarifa zaidi fika:
Benki ya Biashara mkombozi,
Kitalu Na. 40, Nyuma ya Kanisa la Mt. Joseph,
Mtaa wa Mansfield
S.L.P. 38448
DAR ES SALAAM
Namba za simu: +255 22 2137806/7,
Namba ya bure ya maulizo: 0800 750 040
Barua Pepe: info@mkombozibank.co.tz
Tovuti: www.mkombozibank.co.tz
KWA MAELEKEZO YA BODI YA WAKURUGENZI
BALTAZAR B. MBILINYI
KATIBU NA MWANASHERIA WA BENKI
MEI, 2021